IQNA

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah

Vita vya Panga la Quds vimezidisha umoja kote Palestina

12:37 - June 12, 2021
Habari ID: 3473999
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vita vya Saif al Quds (Panga la Quds) vimepelekea kuwepo umoja na mshikamano wa muqawama kote Palestina.

Sheikh Naim Qassim jana Ijumaa aliashiria umuhimu wa mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na kusema kuwa, tangu kuanza Intifadha hadi leo wananchi wa Palestina wamezidisha nguvu na uwezo wao na kuibuka na ushindi. Sheikh Qassim amesema kuwa, wananchi wa Palestina wameshuhudia kuwa Walebanoni wameweza kuibuka na ushindi mbele ya adui Mzayuni kwa kutumia na suhula ndogo kabisa. 

Kiongozi huyo wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, msimu wa mpambano ya mataifa ya Kiarabu umeanza na kwamba Lebanon ile iliyokuwa dhaifu leo hii imepata nguvu kutokana na baraka za muqawama na mapambano. Amesema kumeshuhudiwa baadhi ya matokeo ya muqawama na kusimama kidete katika vita vya Saif al Quds huko Palestina. 

Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, taathira nzuri za vita vya Saif al Quds zitaonekana katika mustakbali na siku zijazo na kwamba vita hivyo vimeimarisha umoja na mshikamano huko Palestina.  

Vita vya Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Ghaza vilianza tarehe 10 mwezi uliopita wa Mei mwaka na kumalizika tarehe 21 mwezi huo huo baada ya  utawala wa Kizayuni wa Israel kuomba kusitisha mapigano na wanamapambano wa Palestina. Vita hivyo vinahesabiwa kua ni ushindi kwa wapigania ukombozi Palestina kwa utawala bandia wa Israel ulilazimika kusitisha vita.

3976783

Kishikizo: palestina ، Quds ، hizbullah ، ghaza
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :