IQNA

Kiongozi Muadhamu awashukuru Wapalestina kwa jumbe zao za pongezi

22:54 - July 12, 2021
Habari ID: 3474095
TEHRAN (IQNA) – Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei imewatumia barua Wapalestina wanaoishi katika kambi za wakimbizi nchini Syria na kuwashukuru kwa jumbe za pongezi kufuatia ushindi katika vita vya Ghaza.

Katika barua hiyo, Ofisi ya Ayatullah Khamenei imewasuhukuru Wapalestina katika kambi za wakimbizi Syria kwa kumtumia salamu za pongezi kufuatia ushindi wa wanamapambano wa Ghaza katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi Mei mwaka huu.

Katika barua kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kirafiki ya Iran na Paestina Mohammad al Buhaisi, mkuu wa masuala ya kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi Muadhamu Hujjatul Islam Mohsen Qumi amemkabidhi ujumbe wa shukrani wa Ayatullah Khamenei.

“Oparesheni ya Upanga wa Quds ilionyesha sehemu ndogo  tu ya nguvu zinazoimarika za harakati ya muqawama.

Katika barua yake, Qumi amesema wanamapambano wa Palestina wameuhami msikiti wa al Aqsa na mji  wa Quds kupitia umoja na mshikamano na hilo linaashiria ushirikiano wa makundi ya muqawama. Aidha amesema vita vya Ghaza mwaka huu vimeweka wazi ukweli kuwa zama za utawala wa Kizayuni wa Israel kutumia mabavu zimefika ukingoni.

Mwezi Mei utawala haramu wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kuwaua Wapalestina zaidi ya 250 wakiwemo wanawake na watoto wengie. Utawala huo ghasibu ulilazimishwa kutangaza usitishaji vita baada ya harakati za ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza kuvurumisha makombora karibu 4000 kuelekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa  jina la Israel.

Baada ya utawala wa Kizayuni kupata pigo katika vita hivyo, ulilazimika kuchukua hatua ya upande mmoja ya kusitihsa mapigano.

3475215

captcha