IQNA

19:50 - July 31, 2021
News ID: 3474144
TEHRAN (IQNA)-Maafisa wa usalama Tunisia Ijumaa walimtia mbaroni mbunge ambaye alikosoa vikali uamuzi wa hivi karibuni wa rais Kais Saied ‘kunyakua; madaraka.

Hivi karibuni rais wa Tunisia alisimamisha bunge kwa muda wa siku 30 kati ya maamuzi mengine ambayo yaliitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.

“Ni mapinduzi ya kijeshi”, alisema mbunge Yassine Ayari kabla ya kukamatwa.

Wakati huo huo, Rais Saied ametangaza kuwa, yeye siyo dikteta na kwamba, hatua alizochukua hivi karibuni nchini humo haziwezi kuhesabiwa kuwa ni mapinduzi.

Rais Saied ambaye hivi sasa anaandamwa na mashinikizo ya ndani na ya nje baada ya kuwatimua kazi mawaziri kadhaa akiwemo Waziri Mkuu na kusimamisha shughuli za Bunge amesema kuwa, hakuna dikteta yeyote kwa sasa nchini humo, uhuru wa kutoa maoni katika nchi hiyo umedhaminiwa na kwamba, hakuna ukwamishaji mambo wowote unaofanyika dhidi ya uhuru wa watu.

Rai wa Tunisia amesisitiza kuwa, ni lazima fedha na mali za nchi hiyo zilizoporwa zirejeshwe kwani kuna mabilioni ya dola yaliyoporwa ambayo ni mali ya watu .

Siku ya Jumapili iliyopita Rais Kais Saied alichukua hatua ya kushtukiza ya kumfuta kazi Spika wa Bunge na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kudhibiti madaraka yote ya nchi.

Wapinzani wake wameitafsiri hatua hiyo kuwa ni mapinduzi baridi aliyofanya kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo. 

Spika wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi amesema hatua aliyochukua Rais Kais Saied ni mapinduzi dhidi ya mapinduzi ya wananchi, katiba ya nchi na uhuru wa taifa.

Hadi sasa miito mbalimbali imetolewa na ingali inaendelea kutolewakieneo na kimataifa ya kutaka mgogoro na taharuki hiyo ya kisiasa iliyotokea Tunisia itatuliwe kwa njia ya mazungumzo na kuzuia kuitumbukiza nchi hiyo ya kaskazini katika vurugu na machafuko.

3475380

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: