IQNA

Binti Mmisri mwenye ulemavu wa macho aliyehifadhi Qu’ani akiwa na umri wa miaka saba

22:12 - August 02, 2021
Habari ID: 3474152
TEHRAN (IQNA)- Binti mmoja nchini Misri ambaye sasa ana umri wa miaka 11 aliweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 7.

Hanine Ashraf Abulaynein ambaye pia alikumbwa na ugonjwa wa saratani akiwa na miaka 9 ni mkazi wa mkoa wa As Sharqiya.

Pamoja na kuwa na changamoto hizo mbili, binti huyo amepata neema ya kuwa mwenye subira na anaendelea kuhifadhi Qur’ani Tukufu na hadi sasa ameshiriki katika mashindano 20 ya Qur’ani Tukufu na kuibuka mshindi.

Mama yake, Bi. Etemad Fathi, 43, anasema bintiye alipata matatizo ya macho akiwa na umri wa miezi 9 na pamoja na hayo alihifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 7.

 

3987821

Kishikizo: misri ، hanine ، qurani tukufu ، kuhifadhi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha