IQNA

Shirika la Kifedha la Kiislamu la Wahed lapata leseni Afrika Kusini

17:44 - August 21, 2021
Habari ID: 3474213
TEHRAN (IQNA)- Shirika la kifedha la Kiislamu la Wahed, ambalo hutoa huduma halali za kifedha limepata leseni ya kutoa huduma nchini Afrika Kusini.

Katika taarifa, shirika hilo limesema Mamlaka ya Sekta ya Kifedha Afrika Kusini (FSCA) imeruhusu Wahed kufungua ofisi zake katika nchi hiyo.

Shirika la Kifedha la Wahed linawalenga wawekezaji Waislamu ambao wanataka huduma za kifedha zinazoenda sambamba na mafundisho ya Kiislamu. Tayari shirika hilo, ambalo lina makao yake makuu New York Marekani, limeshaanza oparesheni pia nchini Uingereza na halikadhalika katka nchi za Indonesia, Nigeria na India.

Mkurugenzi wa Wahed Junaid Wahedna anasema, "Tunataraji kuwa na taathira nchini Afrika Kusini."

Shirika la Kifedha la Wahed lilianzishwa mwaka 2015 na lina wateja zaidi ya laki mbili duniani kote. Katika kipindi hicho shirika hilo limeweza kupata dola milioni 40 kutoka wawekezaji mbali mbali.

/3992007

captcha