IQNA

13:37 - August 26, 2021
Habari ID: 3474227
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa na baraza lake la mawaziri wamefika katika Haram Takatifu ya muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomieni -Mwenyezi Mungu Amrehemu-na kujadidisha bai'a na mkono wa utii kwa malengo ya Imam na Mapinduzi ya Kiislamu.

Rais Ibrahim Rais na baraza lake la mawaziri la serikali ya 13 mapema leo asubuhi wamefika katika haram ya Imam Khoemini kusini mwa Tehran sambamba na kuanza 'Wiki ya Serikali' na pia kuanza rasmi baraza jipya la mawaziri. 

Katika hotuba yake akiwa hapo, Rais Raisi amesisitiza kuhusu nafasi ya wananchi katika fikra za Imam Khomeini (MA) na kusema fikra za Imam kuhusu nukta hiyo zilikuwa tafauti na za wanasiasa wa kawaida. Ameongeza kuwa serikali yake inataka wananchi wahisi kuwa serikali iko pamoja nao na inawahudumia bila kujadili mitazamo yao ya kisiasa.

Jana Jumatano, wabunge katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu,  Bunge la Iran, waliipigia kura ya kuwa na imani na serikali mpya ya Rais Ibrahim Raisi na kuwapasisha mawaziri 18 kati ya 19. Waziri pekee ambaye mawaziri hawakumuafiki kutokana na uzoefu mdogo wa utendaji ni waziri wa elimu.

Akizungumza mara baada ya kupasishwa mawaziri hao, Rais Ibrahim Raeis amelipongeza Bunge kwa kupasisha mawaziri wake kwa wingi mkubwa wa kura na kueleza kwamba, hatua hiyo ni mwanzo mzuri wa ushirikiano wa Serikali na Bunge kwa ajili ya kuijenga Iran yenye nguvu.

Aidha akizungumza leo Alhamisi katika kikao chake cha kwanza na baraza lake la mawaziri, Sayyid Ibrahim Raisi amesema, wananchi wa Iran wanapaswa kuhisi ustawi na maendeleo pamoja na utekelezwaji wa uadilifu. Amesema kuwa, katika baadhi ya sekta kuna hali ya kubakia nyuma kukubwa ambako kunapaswa kufidiwa.

3993178

Kishikizo: imam khomeini ، iran ، ibrahim raisi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: