IQNA

Rais wa Iran afika bungeni kutetea baraza lake la mawaziri

17:30 - August 21, 2021
Habari ID: 3474212
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi anasema amechagua baraza la mawaziri ili kuboresha uchumi na kupambana na ufisadi.

Ameyasema hayo mapema leo wakati Bunge lilipoanza kujadili majina ya mawaziri walioteuliwa na Rais mpya wa Iran.

Rais Ebrahim Raisi wa Iran ameeleza muhtasari wa mipango ya baraza la mawaziri lijalo, akisema limebuniwa kuhakikisha haki na maendeleo nchini Iran.

Amesema huu ni wakati wa kufanya harakati ya kijihadi na ya wananchi kwa ajili ya kujenga Iran imara na yenye nguvu. 

Ameshiria juhudi zinazolenga kudhibiti janga la virusi vya corona kama kipaumbele cha juu cha serikali mpya na kusema miongoni mwa ajenda kuu za serikali ni kustawisha uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi.

Rais Raisi alisema orodha ya mawaziri waliopendekezwa inajumuisha mawaziri vijana na wenye uzoefu, ambao sifa yao kuu ni kujitolea, kuchapa kazi kwa bidii na kupambana na ufisadi.

Rais Ebrahim Raisi ameongeza kuwa mipango ya muda mfupi na wa kati imeandaliwa ili kushughulikia matatizo yanayoikali nchi.

Vilevile ametilia mkazo udharura wa kustawishwa uhusiano kimataifa na kujali maslahi ya kitaifa. 

3991983

captcha