IQNA

11:33 - September 21, 2021
News ID: 3474321
TEHRAN (IQNA) – Hafla imefanyika katika mji wa Khan Yunis katika eneo la Palestina la Ukanda wa Ghaza kwa lengo la kuwaenzi wanafunzi waliohifadhi Qur’ani Tukufu.

Jumla ya wanafunzi 350 ambao wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu au baadhi ya Juzuu wameenziwa na kupongezwa kwa jitihada zao katika mahafali iliyofanyika Ijumaa.

Mafanikio hayo yanajiri pamoja na kuwa Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wako chini ya mzingiro wa kinyama wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tokea mwaka 2007, utawala haramu wa Israel, kwa kushirikiana na utawala wa Misri, uliweka mzingiro wa anga, nchi kavu na baharini dhidi ya Ukanda wa Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuichagua kidemokrasia harakati ya Hamas kuongoza eneo hilo. Mzingiro huo umelifanya eneo hilo lenye watu karibu milioni moja na nusu kutajwa kuwa gereza kubwa zaidi la wazi duniani.

Mwezi uliopita, kiongozi mwandamizi wa Hamas Yahya Sinwar alisema wananchi wa Palestina wamekaribia sana kuuvunja mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kushirikiana na Misri tokea mwaka 2007.

Mbali na mzingiro huo, utawala haramu wa Israel pia umeanzisha vita mara kadhaa dhidi ya Ghaza tokea mwaka 2008 ambapo maelfu ya Wapalestina wakiwemo wanawake na watoto wameuawa.

3998880

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: