Majid Namjoo, katibu wa Kamati ya Iran ya Ushiriki wa Umma, Malazi na Lishe katika Arbaeen, aliongeza kuwa Mawikb zilisambaza milo milioni 113 ya chakula miongoni mwa waombolezaji.
Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wengine wote katika eneo husika wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) n.k na pia kupata sehemu ya kupumzika.
Alipongeza jitihada za dhati za watumishi wa Mawkib na kutoa ripoti kuhusu utendaji wa Kamati hiyo wakati wa Arbaeen ya mwaka huu wa 1447 Hijria Qamaria sawa na 2025.
Akisisitiza kuwa wenyeji wakuu wa matembezi na Ziyara ya Arbaeen ni wananchi wema na serikali ya Iraq, aliongeza kuwa uwepo wa Mawkiba za Kiarani kando na zile za Iraq ni kwa lengo la kushiriki baraka za kuwakrimu wageni wa Arbaeen.
Alisema mwaka huu, Mawkib 1,526 za Kiarani nchini Iraq na Mawkiba 1,225 nchini Iran zilikaribisha waombolezaji wa Arbaeen.
Namjoo alisema Makao Makuu ya Iran ya Maendeleo na Ujenzi wa Atabat (makaburi matukufu), kwa kupanga masuala na kuratibu na mashirika husika nchini Iran na Iraq, yaliandaa mazingira yanayohitajika kuwezesha usafiri wa malori 7,553 yaliyojaa vifaa na bidhaa kwa ajili ya maandamano ya Arbaeen.
Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa hasa na Waislamu Shia siku arobaini baada ya Siku ya Ashura, likikumbuka kifo cha kishahidi cha Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Shia.Aliuawa shahidi Karbala, Iraq mwaka wa 61 Hijria Qamaria.
Ni moja ya misafara mikubwa ya kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu Shia, pamoja na Waislamu Sunni na wafuasi wa dini nyingine, hufika Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen ilisadifiaana na Agosti 14.
3494391