IQNA

Ndege za kivita za Israeli zahujumu Ukanda wa Ghaza

22:27 - August 29, 2021
Habari ID: 3474236
TEHRAN (IQNA)- Ndege za kivita zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni wa Israeli zimetekeleza mashambulio ya angani kati mwa Ukanda wa Gaza

Duru za habari Palestina zinadokeza kuwa ndege zisizo na rubani zililenga barabara ya Salah al-Din, ambayo ni barabara kuu ya Gaza, mapema Jumapili.

Hujuma hiyo imekuja  masaa kadhaa baada ya ripoti kusema kuwa Wapalestina wengine 11 wamejeruhiwa wakati wa shambulio  la utawala huo dhidi ya maandamano katika eneo la pwani ya Ghaza.

Wizara ya afya ya Ghaza imesema Wapalestina walijeruhiwa baada ya jeshi la Israeli kuanza kuwapiga risasi waandamanaji katika sehemu ya mashariki mwa pwani ya Ghaza.

Ukanda wa Ghaza umekuwa chini ya mzingiro wa mara kwa mara wa Israeli na uchokozi unaofanana tangu 2007, wakati harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina ya Hamas ilipochaguliwa kidemokrasia kuongoza eneo hilo.

3475582

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza palestina
captcha