IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Masuala ya Afghanistan na Iraq ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiislamu

14:30 - November 12, 2021
Habari ID: 3474545
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema leo masuala ya Iraq na Afghanistan ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria maudhui mbili za leo za ulimwengu wa Kiislamu yaani Iraq na Afghanistan na kusema, madola ya kibeberu yanataka kuona ulimwengu wa Kiislamu ukisambaratika.

Akiashiria kadhia ya Iraq, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema yanayojiri Iraq ni muhimu kwa ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa maadui wanalenga kuvuruga na kuusambaratisha ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha amesema hujuma ya hivi karibuni  iliyolenga nyumba ya Waziri Mkuu wa Iraq ni yenye kutiliwa shaka huku akitoa wito kwa wakuu wa Iraq kutatua mgogoro wa matokeo ya uchaguzi kwa njia za kisheria.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema Marekani imetoroka Afghanistan lakini njama zake za kuibua hitilafu na mifarakano katika nchi hiyo zingali zinaendelea.

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameashiria hali ya mambo nchini Afghanistan na kuongeza kuwa, Iran ina hamu ya kuona Afghanistan huru, yenye kujitegemea na yenye nguvu ambayo iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Wazayuni na Marekani. Aidha amesema Iran inataka kuhakikisha kuwa usalama wa mipaka yake unalindwa na halikadhalika pia haki za Mashia wa Afghanistan zinalindwa. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran pia amesisitiza umuhmu wa kuundwa serikali inayojumuisha makundi yote ya Afghanistan.

4012524/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha