IQNA

Uhasama wa Australia dhidi ya Hizbullah walaaniwa

15:44 - November 25, 2021
Habari ID: 3474599
TEHRAN (IQNA)- Australia imelaaniwa vikali kufuatia hatua yake ya kutangaza chama cha Hizbullah cha Lebanon kuwa eti ni harakati ya kigaidi.

Harakati ya Hizbullah imetoa taarifa na kulaani vikali uamuzi wa serikali ya Australia wa kukiweka chama hicho katika orodha ya makundi ya kigaidi na kusema hatua hiyo ni kujidhalilisha nchi hiyo mbele ya matakwa ya Marekani, utawala wa Kizayuni na sera za ugaidi na mauaji.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Manar, Hizbullah imetoa taarifa na kulaani uamuzi huo wa Australia na kuongeza kuwa: "Uamuzi huo na maamuzi mengine kama hayo ya baadhi ya nchi za Magharibi hayatakuwa na taathira katika moyo wa taifa tiifu la Lebanon wala moyo wa wapigania uhuru."

Hizbullah imeendelea kusema katika taarifa hiyo kuwa, "uamuzi wa Australia hautabadilisha msimamo wa harakati hiyo katika mapambano au muqawama na kuihami Lebanon na watu wake na hali kadhalika uungaji mkono kwa harakati zinazokabiliana na utawala ghasibu na vamizi wa Kizayuni."

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Australia kutangaza Jumatano kuwa imeiweka Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Uamuzi huo wa Australia umekuja kufuatia mashinikizo ya mashirika ya Kizayuni na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa miaka kadhaa sasa Marekani na utawala wa Kizayuni zimekuwa zikifanya jitihada za kupunguza umashuhuri wa Hizbullah nchini Lebanon.

Wakati huo huo, Harakati ya Jihad Islami ya Palestina uamuzi huo wa Australia umetokana na mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jihad Islami inasema Hizbullah inatekekeleza mapambano halali ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Nayo Harakati ya Ansarullah ya Yemen imelaani vikali hatua hiyo ya Australia huku ikitoa wito kwa Waislamu kuchukua hatua za kivitendo za kukabiliana na maamuzi hayo yaliyojaa uhasama dhidi ya harakati za muqawama katika eneo.

4016122

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha