IQNA

Rais Putin wa Russia asema Hizbullah ni nguvu muhimu katika siasa za Lebanon

10:10 - October 22, 2021
Habari ID: 3474455
Rais Vladimir Puton wa Russia amesema harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ina nafasi muhimu katika uga wa kisiasa nchini Lebanon.

Ameyasema hayo Alhamisi katika kikao cha Klabu ya Mazungumzo ya Valdai katika mji wa Sochi nchini Russia na kuongea kuwa: "Nafahamu vyema kuwa watu tafauti katika nchi tafatui wana mitizamo tafauti kuhusu Hizbullah."

Putin amesema kwa matazamo wa Russia, Hizbullah ni nguvu muhimu ya kisiasa nchini Lebanon na kuongeza kuwa, Russia inawasiliana na makundi yote yenye nguvu za kisiasa Lebanon na itaendelea kufanya hivyo.

Aidha amesema Russia inataka kuona pande zote za kisiasa Lebanon zinafikia mapatano bila mapigano na kuongeza kuwa, Moscow inashirikiana na Walebanon wote kuzuia umwagikaji damu nchini humo.

Kauli ya Putin imekuja baada ya watu saba kuuaa shahidi na wengine 60 kujeruhiwa Oktoba 14 wakati wafuasi wa Hizbullah walipokuwa wakiandamana kwa amani dhidi ya jaji anayechunguza mliuko katika Bandari ya Beirut mwaka jana ambaye anatuhumiwa kupendelea upande moja. Waliouawa katika hujuma hiyo aghalabu walikuwa ni wafuasi wa Harakati ya Hizbullah.

Putin amesema hawezi kutoa tamko kuhusu masuala ya kisiasa yanayofungamanishwa na idara ya mahakama ya Lebanon lakini ameongeza kuwa, mlipuko wa Bandari ya Beirut unahusishwa na baadhi waliotaka kupata faidi kwa kuuza fataliza kwa bei ya juu.

4007002

Kishikizo: hizbullah ، beirut ، vladimir putin ، russia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha