IQNA

Muqawama

Kiongozi wa Ansarullah: Utawala wa Kizayuni unalenga kuteka maeneo zaidi hadi nje ya Syria

17:50 - December 14, 2024
Habari ID: 3479899
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni unakodolea macho ya tamaa maeneo yote yanayopakana na ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu yakiwemo ya Syria na Misri na kusema kuwa, Netanyahu anatumia vibaya matukio ya Syria ili kutimiza njama hizo za muda mrefu za Kizayuni.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amezungumza moja kwa moja Ijumaa kuhusiana na matukio ya hivi karibuni ya nchi yake, ya Syria na Palestina hasa Ukanda wa Gaza.

Sayyid Abdul Malik Badr al-Din al-Houthi amesema katika hotuba yake hiyo kwamba: Adui Mzayuni kila siku anafanya mauaji makubwa dhidi ya wananchi wa Palestina na matokeo yake ni kwamba Wapalestina 1,800 wameshauawa shahidi au kujeruhiwa tangu mwanzoni mwa wiki hii.

Ameongeza kuwa: Shambulio la utawala wa Kizayuni katika hospitali ya Kamal Adwan kwa kila aina ya silaha linaonyesha ukatili wa kuchupa mipaka na usiotasawirika wa utawala huo dhalimu na ilikuwa kana kwamba unashambulia ngome imara ya kijeshi. Kukilenga moja kwa moja kituo cha oksijeni cha Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza na kuua watoto wanaosaidiwa kupumua kwa oksijeni pamoja na wagonjwa wengine mahututi, ni ukatili wa Israel ambao haujawahi kuripotiwa katika historia.

Vile vile amezungumzia matukio ya Syria na kusema: Adui Mzayuni anayachukulia matukio ya Syria kuwa ni fursa ya kuvuruga usalama na hasa katika nchi zinazopakana na ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu kama Syria na Misri. Amesema: Adui anafanya njama kwa kushirikiana na Marekani za kuzidi kuwagombanisha Waislamu na kufanikisha siasa zake za kujitanua. 

4253869

Habari zinazohusiana
captcha