IQNA

Ireland yatoa idhini ya kujenga msikiti na kituo cha Kiislamu

21:08 - November 26, 2021
Habari ID: 3474603
TEHRAN (IQNA)- Idhini imetolewa kwa ajili ya kujenga Msikiti na Kituo cha Kiislamu cha Mji wa Limerick nchini Ireland.

Kwa mujibu wa taarifa, idhini imetolewa kwa ajili ya mradi huo wa Kundi la Dawat-e-Islami ambao utakuwa na jengo lenye ghorofa tatu.

Inatazamiwa kuwa, idadi kubwa ya Waislamu watakuwa wakishiriki katika Sala msikitini hapo kila siku ambapo na sasa hakutakuwa na uhaba wa nafasi hasa wakati wa Sala za Ijumaa na  Idi.

Wasimamizi wa mradi huo wanasema wanalenga kujenga kituo cha Kiislamu cha utamaduni ambacho kitawahudumia Waislamu na wasiokuwa Waislamu.

Mji Limeric una Waislamu wengi ambao kwa sasa huswali katika msikiti ulio katika mtaa wa Windmill na nafasi hiyo haitoshi Waislamu wanaozidi kuongezeka.

3476661

Kishikizo: ireland waislamu msikiti
captcha