IQNA

Maafisa wa Polisi Waislamu Ireland Waruhusiwa kuvaa Hijabu

13:36 - April 06, 2019
2
Habari ID: 3471900
TEHRAN (IQNA)- Idara ya Polisi nchini Ireland imeamua kuwaruhusi maafisa wa polisi kike ambao ni Waislamu kuvaa vazi la staha la Hijabu.

"Ni matumaini yangu kuwa hatua hii itawahimiza wa raia wa jamii za waliowachache kujiunga na kikosi cha An Garda Síochána (Kikosi cha Polisi cha Jamhuri ya Ireland)," amesema mkuu wa kikosi hicho, Kamishna Drew Harris. Halikadhalika amesema Masingasinga nao pia wataruhusiwa kuvaa vilemba kama sare ya polisi.

Katika taarifa rasmi, Idara ya Polisi nchini Ireland imesema hatua hiyo inaendana na maamuzi sawa na hayo yaliyochukuliwa na idara za polisi za nchi zingine za Kimagharibi kama vile Scotland, New Zealand, Uingereza, Australia na Canada.

Ameongeza kuwa, wanalenga kuzihakikishia jamii za wachache nchini humo kuwa Idara ya Polisi ni shirikishi katika ajira na inalipa uzito suala la kuwa na maafisa wa jamii zote.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2016, idadi ya Waislamu nchini Ireland inakadiriwa kuwa 65,000 kati ya watu wote takribani milioni 4.8.

/3468225

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Haji Ally
0
0
Ni mpango mzuri kabisa wa kuunganisha itikadi zote bila ubaguzi. Hongera sana kwa jamhuri ya ireland.
Haji Ally
0
0
Ni mpango mzuri kabisa wa kuunganisha itikadi zote bila ubaguzi. Hongera sana kwa jamhuri ya ireland.
captcha