IQNA

Watetezi

Rais wa zamani wa Ireland alaani unafiki wa kimataifa kuhusu jinai za Israel

17:07 - October 05, 2024
Habari ID: 3479539
IQNA-Rais wa zamani wa Ireland amekosoa jibu la jamii ya kimataifa kwa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na Lebanon.

Akizungumza Ijumaa, Mary Robinson ameulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutenda jinai bila kuadhibiwa katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), huku akikosoa nchi za Magharibi, hasa Marekani kwa kushindwa kuzuia jinai hizo.

Maoni yake yamekuja huku kukiwa na hali ya wasiwasi katika eneo la Magharibi mw Asia, ambapo mashambulizi ya anga ya Israel yameendelea kwa siku kadhaa dhidi ya eneo la kusini mwa Beirut na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Akizungumza katika mahojiano na Radio RTE ya  Ireland, Robinson, anayewakilisha taasisi ya The Elders - ambayo ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa lililoanzishwa na Shujaa Nelson Mandela na Richard Branson- amesisitiza haja ya pande zote katika Asia Magharibi kujizuia kueneza zaidi taharuki.

Robinson amesema jamii ya kimataifa imeonyesha ubaguzi baina ya raia wa Israel na Palestina ambapo amesema Waisraeli walitetewa wakati wa mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran lakini  raia wa Palestina na Lebanon hawatetewi wakati wanaposhambuliwa na utawala wa Israel.

Robinson amemkosoa hasa Rais wa Marekani, Joe Biden, kwa kuendelea kuipatia Israel silaha licha jinai za utawala huo unaokiuka sheria za kimataifa katika Ukanda wa Gaza.

Katika matamshi yake, Robinson amelaani vikali jinai za Israel huko Gaza, ambapo utawala huo "umeua watu karibu 42,000 na kujeruhi wengine wengi hasa watoto tangu Oktoba 7, 2023.

Rais wa zamani wa Ireland amesema kuwa Israel sasa imeendeleza jinai zake kwa kuwalenga watu wa Lebanon huku ikipanga mashambulizi dhidi ya Iran.

3490139

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ireland gaza palestina
captcha