Katika mahojiano na televisheni ya Al Mayadeen ya Lebanon, Muhammed al Bukhaiti amesema, 'masaa yajayo yatakuwa muhimu katika vita vya Ma'rib"
Al Mukhaiti ameongeza kuwa, Jeshi la Yemen liko chini ya mashinikizo ya wananchi kukomboa mkoa wa Ma'rib ambao unakaliwa kwa mabavu na wanamgmabo wanaopata himaya ya Saudi Arabia.
Siku ya Jumatano, duru katika medani za vita Ma'rib ziliidokezea televisheni ya Al Mayadeen kuwa askari wa Jeshi la Yemen wakishirikiaana na wapiganaji wa Kamati za Kujitolea za Wananchi wamechukua udhibiti wa eneo la milima la al Balaq al Sharqiya katibu na mji wa Ma'riba Kwa mujibu wa duru za kijeshi al- Balaq al Sharqiya "ni miinuko ya mwisho ya kuulinda mji wa Ma'arib kutoka upande wa kusini mashariki."
Duru za usalama zinadokeza kuwa wanamgambo wanaopata himaya ya Saudi Arabia wametoroka medani za vita na kwamba baada ya 'siku chache, mji wa Ma'rib utakombolewa kwa ushirikiano wa Jeshi la Yemen na Kamati za Wananchi.:
Kwingineko, al-Bukhaiti amesema kushindwa wapiganaji wanaopata himaya ya Saudia huko Ma'rib kunamaanisha kushindwa Saudia katika medani zilizosalia Yemen. Aidha amesema kukombolewa mkoa wa Ma'rib ni jinamizi kwa Saudia Arabia katika vita vya Yemen.
Afisa huyo wa Ansarullah amefafanua kuwa, kukombolewa Ma'rib kutaandaa mazingira ya kuondolewa mzingiro wa Saudia dhidi ya Yemen kwani nchi wanachama wa muungano vamizi wa Saudia hazitaweza tena kufanikisha mzingiro au vita dhidi ya Yemen.
Mkoa wa Ma'rib, ambao mji wake mkuu ni Ma'rib, uko kati kati ya mikoa kadhaa ya Yemen na unatazamiwa kama stratijia ya oparesheni za kukomboa Yemen tokea mwaka jana.
Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Saudia ilipata himaya ya Marekani, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu katika vita dhidi ya Yemen, ambayo ni nchi masikini zaidi katika Bara Arabu.
Lengo la vita hivyo lilikuwa ni kuiondoa madaraknai harakati ya Ansarullah lakini Wasaudi wameshindwa kufikia lengo hilo. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.
Hadi hivi sasa uvamizi huo wa Saudia na waitifaki wake umeshasababisha makumi ya maelfu ya Wayemen kuuawa, wengine wengi kujeruhiwa huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.