IQNA

Saudia yatangaza kuendelea marufuku kugusa Hajar Al aswad

15:41 - December 20, 2021
Habari ID: 3474699
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Hija na Umrah Saudi Arabia imetangaza kuendelea marufuku ya kugusa Hajar Al Aswad (Jiwe Jeusi) na kuswali katika Hijr Ismail katika Msikiti Mtakatifu wa Makka.

Wizara ya Hija na Umrah imetangaza kuwa hakutakuwa na huduma itakayoongezwa katika aplikesheni ya Eatmarna kuhusu kubusu Hajar al Aswad.

Jiwe hilo liko katika pembe moja upande wa Mashariki/Kusini mwa Ka'abah. Urefu wake kutoka ardhi na takriban mita moja na nusu. Jiwe hilo limefunikwa na chuma cha fedha safi kabisa. Tunaloliona ni karibu na nusu ya jiwe tu, na zaidi ya nusu nyingine imefunikwa ndani hatuioni. Eneo hilo lina umuhimu katika historia ya Uislamu.

Wizara ya Hija ya Saudia inasema kwa sasa kulibusu Jiwe Jeusi kunategemea kanuni zilizowekwa na Idara ya Usiamamizi wa Misitikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina.

Awali wizara hiyo ilikuwa imetangaza kuwa wanaotekeleza Hija Ndogo ya Umrah wanaweza kuwasilisha maombi ya kubusu Jiwe Jeushi au kugusa Al Rukn Al Yamaani pamoja kuswali katika eneo la Hijr Ismail katika Msikiti Mtakatifu wa Makka. Hatahivyo sasa haiwezekani kufanya hivyo kutokana na kile kinachoonekana ni kuzuia maambukizi ya Corona.

3477007

Kishikizo: umrah jiwe jeusi saudia
captcha