IQNA

Hatua kali misikitini Saudia kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

18:20 - December 24, 2021
Habari ID: 3474717
TEHRAN (IQNA)- Misikiti kote Saudi Arabia imetakiwa kuchukua hatua kali za kuhakikisha kuwa wote wanaoshiriki katika ibada wanatekeleza kanuni za kukabiliana na COVID-19.

Amri imetolewa na Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia Abdulatif Aal Sheikh kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19 katika ufalme huo. Katika dikrii yake, ametaka wasimamizi wa misikiti kuhakikisha wanaoshiriki katika ibada wanazingatia kanuni zote za kiafya hasa uvaaji barakoa na kutokaribiana ili kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Agizo hilo limetolewa baada ya kubainika kuwa watu wanapuuza kanuni zilizowekwa misikitini kuhusiana na maambukizi ya COVID-19 na hivyo kuchangia ongezeko la maambukizi.

Siku ya Alhamisi Saudi Arabia iliripoti maambukizi mapya 287 ya corona huku mtu moja akipoteza maisha. Hadi sasa walioambukizwa corona Saudia ni 551,749 na walipoteza maisha ni 8,868.

3477065

captcha