IQNA

19:26 - March 07, 2021
News ID: 3473712
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran imeanza Jumamosi Machi 6 katika sherehe iliyoudhuriwa na Mkuu wa Shirika la Iran la Wakfu na Misaada Hujjatul Islam wal Muslimin Mehdi Khamoushi.

Aidha sherehe ya kuanza fainali hiyo imeudhuriwa pia na Katibu wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni Iran Hujjatul Islam wal Muslimin Saeed Reza Ameli.

Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani kutokana na janga la  COVID-19 au corona, yanafanyika kwa njia ya intaneti.

 
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: