IQNA

Waliomuua Luteni Jenerali Soleimani lazima wafikishwe mahakama ya kimataifa

12:51 - December 23, 2021
Habari ID: 3474713
TEHRAN (IQNA) – Msomi mmoja wa Algeria amesisitiza kuwa wale waliomuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani lazima wafikishwe kizimbani.

Akizungumza katika warsha ya "Shahidi Qassim Soleimani na Heshima ya Kiislamu", Yusuf Houri amesema waungaji mkono wa mapambano ya Kiislamu au muqawama wanafuatilia kadhia ya kuuawa shahidi kamanda huyo Muirani ili waliomuua wafikishwe katika mahakama za kimataifa.

Warsha hiyo iliandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Algeria na Chuo Kikuu cha Imam Sadiq AS.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
Houri ambaye ni mhadhiri wa sheria katika Chuo Kikuu cha Algeria ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kupambana na maadui wa Umma wa Kiislamu na kuunga mkono ukombozi wa Palestina na Quds Tukufu. Amesema ni lazima Marekani ijibu mashtaka ya kuhusika na mauaji ya kamanda huyo Muirani kwani kitendo hicho likuwa ni jinai ya kivita.

Katika kutekeleza ahadi yake ya kulipiza kisasi kikali kwa Marekani kutokana na nchi hiyo kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na shakhsia wengine aliokuwa nao, Iran ilishambulia kwa makombora kambi ya kijeshi ya askari gaidi wa Marekani ya Ain Assad nchini Iraq.

4022561

  

Kishikizo: Soleimani iran
captcha