IQNA

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran

Iran itawasaka wote waliomuuwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani

18:30 - January 03, 2022
Habari ID: 3474760
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa Serikali, Idara ya Mahakama na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran zinapasa kutumia vyombo vyote vya kisheria kwa ajili ya kuwafuatilia wahusika wa mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qasem Soleimani.

Hujjatul Islam Walmuslimin Gholam-Hossein Mohseni-Eje'i ambaye leo alihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Idara ya Mahakama ya Iran kwa mnasaba wa  kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani, ameeleza kuwa: Haj Qasem Soleimani alikuwa akipambana waziwazi na kwa ujasiri na ushujaa na magaidi wa kundi la Daesh (ISIS), adui Mzayuni na Marekani na alikuwa akitia wasiwasi na hofu kubwa katika moyo wa adui katika medani za vita, na wakati huo huo alikuwa mnyenyekevu kwa wananchi.  

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amebainisha kuwa, hii leo wapenda haki na wapigania ukombozi duniani kote wanamtambua Luteni Jenerali Soleimani kama shakhsia aliyekuwa mstari wa mbele katika medani ya mapambano dhidi ya magaidi na mabeberu wa dunia na kwamba akthari ya watu duniani nyoyo zao ziliangaziwa na nuru ya Uislamu walipobainishiwa ushujaa na ujasiri wa Haj Qasem Soleimani dhidi ya magaidi hao makatili kwa kuelewa jinsi askari wa ngazi ya juu wa Uislamu alivyokimbilia kuwasaidia watu wanaodhulumiwa. 

Mohseni Eje'i ameeleza kuwa, viongozi watenda jinai wa Marekani walimuua kinara wa mapambano dhidi ya ugaidi kwa mauaji yao dhidi ya Kamanda Soleimani na kuongeza kuwa: Wamarekani watenda jinai watalipizwa kisasi cha mauaji hayo kwa mikono ya wanajihadi wenzake na hawatapata tena usingizi mnono. Amesema popote pale walipo lazima mioyo yao itetemeke kwa kuandamwa na vikosi vya wanamuqawama.

Wakati huohuo Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amepongeza hatua za Mkuu wa Mahakama na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Tehran za kuwafuatilia wahusika wa mauaji ya Luteni Jenerali Soleimani na kueleza kuwa, tayari zimefunguliwa kesi za jinai ili kufuatilia faili la mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Soleimani na wanajihadi wenzake na vikao mbalimbali vimeshafanyika pia kati ya Iran na maafisa wa vyombo vya sheria wa Iraq.

Itakumbukwa kuwa Jumatatu ya leo ambayo ni tarehe 3 Januari, inasadifiana na mwaka wa pili tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC. Shujaa huyo aliuawa kidhulma uraiani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq. Aliuawa shahidi kwa amri ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump akiwa pamoja na wanamuqawama wenzake tisa akiwemo Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu wa Mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashdu al Shaabi.

4025864

Kishikizo: Soleimani iran irgc EJEI
captcha