IQNA

Ripoti: Utawala wa Kizayuni uliwaua raia 357 Wapalestina mwaka 2021

9:39 - January 02, 2022
Habari ID: 3474754
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwaua raia Wapalestina wasiopungua 357 mwaka 2021 huku jamii ya kimataifa ikiwa kimya kuhusu jinai hizo dhidi ya raia.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Jumuiya ya Kitaifa ya Familia za Mshahidi Palestina. Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Muhammad Sbeihat amesema ripoti hiyo imetegemea utafiti ambao ulifanyika katika maeneo yote ya Palestina.

Ripoti hiyo inaonyesha asilimia 19 ya raia waliouawa ni wanawake, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya wanawake kuuawa tokea utawala bandia wa Israel uasisiwe mwaka 1948 baada ya kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Halikadhalika ripoti hiyo imebaini kuwa asilimia 22 ya waliouawa shahidi walikuwa ni watoto huku na jinai hiyo imewezekana kwa sababu jamii ya kimataifa imenyamaza kimya na haichukui hatua zozote dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sbeihat aidha ametoa wito kwa jamii ya kimataifa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuchukua hatua za kisheria za kufuatilia jinai za Israel katika mahakama za kimataifa.

Wanajesthi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamekuwa wakiwaua kiholela Wapalestina ambao wanajitokeza kupinga ardhi zao kuendelea kukaliwa kwa mabavu na walowezi wa Kizayuni.

Hayo yanajiri wakati ambao, Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema katika ripoti yake kwamba, vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na Israel vimeshadidi mno tangu kuanza mwaka huu wa 2021.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mwaka uliopita wa 2020 utawala wa Kizayuni wa Israel ulibomoa nyumba karibu 689 katika Ukingo wa Magharibi na Quds tukufu na kulazimisha mamia ya familia za Wapalestina kuwa wakimbizi. 

3477185

captcha