IQNA

Watetezi wa Palestina

Wayemen waandamana kuunga mkono Palestina na kupinga Wazauni na Marekani

19:20 - December 07, 2024
Habari ID: 3479868
IQNA-Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano mapya ya kila wiki katika mji mkuu Sana'a na miji kadhaa nchini humo kusisitiza uungaji mkono wao kwa Wapalestina wanaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel.

Siku ya Ijumaa, Wayemen walikusanyika katika maandamano makubwa Sana'a na majimbo mengine, ikiwa ni pamoja na Sa'ada, Hudaydah, Hajjah, Ibb, al-Bayda, Amran, Jawf, Dhamar na Ta'izz, ikiwa ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina, huku wakiwapongeza wanamuqawama wa Palestina kwa kusimama kidete dhidi ya Wazayuni.

Wakiwa wamebeba bendera za Yemen na Palestina, waandamanaji hao walipiga nara kama vile "Ewe Gaza, Ewe Palestine... Wayemeni wote wako pamoja nawe"n "Utawala wa Uhalifu Utatoweka... na "ushindi utakuwa wa jeshi la al-Qassam," wakiashiria tawi la kijeshi la harakati ya muqawama wa Palestina Hamas.

Pia wamepongeza oparesheni za hivi karibuni dhidi ya Israel zilizofanywa na wapiganaji wa Iraq na Yemen, wakieleza kuunga mkono operesheni za kulipiza kisasi zinazofanywa na vikosi vyao vya kijeshi.

Vikosi vya jeshi la Yemen siku ya Jumanne vilitangaza kutekeleza operesheni tatu za pamoja za kijeshi huku muqawama wa Iraq ukilenga ngome za utawala haramu wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Operesheni hizo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za harakati za muqawama katika eneo kwa ajili ya kukabiliana na jinai za Isarel dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza.

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba 2023 na hadi sasa yamesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 44,600 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine zaidi ya 105,800. Maelfu zaidi pia wametoweka na inakisiwa kuwa wamekufa chini ya vifusi.

3490957

Habari zinazohusiana
captcha