IQNA

Hamas: Watenda jinai wanaoua watoto, wanawake Ghaza hawatakwepa mkono wa sheria

17:11 - December 27, 2021
Habari ID: 3474731
TEHRAN (IQNA)- Waliotenda jina katika Vita vya Furqan (vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza mwaka 2008-2009) hawataruhusiwa kukwepa mkono wa sheria, imesisitiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

Katika taarifa kwa mnasaba wa vita hivyo ambavyo pia ni maarufu kama Vita vya Siku 22, Hamas imeapa kuhakikisha kuwa waliohusika katika mauaji ya watoto na wanawake wa Ghaza watafikishwa kizimbani.

Taarifa hiyo imesema jinai hizo haziwezi kusahaulika na Wapalestina hawatawassamehe watenda jinai.

Ikumbukwe kuwa, Katika siku kama ya leo miaka 13 iliyopita, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilianzisha hujuma kubwa na ya pande zote katika Ukanda wa Ghaza magharibi mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Wakazi wa eneo hilo waliwakasirisha viongozi wa Kizayuni kutokana na kupambana kwao kishujaa dhidi ya uchokozi na mashambulizi ya Wazayuni na pia hatua yao ya kuiunga mkono serikali halali ya Palestina iliyokuwa ikiongozwa na harakati ya Hamas.

Ni kwa sababu hiyo ndio maana Ukanda wa Ghaza ukawekwa chini ya mzingiro wa kiuchumi wa utawala haramu wa Israel kwa karibu mwaka moja na nusu kabla ya mashambulizi hayo, mzingiro ambao unaendelea kuwasababishia Wapalestina wa eneo hilo matatizo chungu nzima kama vile ukosefu wa chakula na dawa.

Vita hivyo vya siku 22 vilianza Disemba 27 , 2008 na kuendelea hadi Januari 18 2009. Kwa mujibu wa taarifa jeshi katili la Israel liliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia katika vita hivyo mbali na kutekeleza uharibifu mkubwa.

4023982

captcha