IQNA

Watu 10 wauawa katika hujuma ya magaidi wa Al Shabab mjini Mogadishu

18:58 - January 12, 2022
Habari ID: 3474796
TEHRAN (IQNA)- Watu wasiopungua 10 wameuawa katika hujuma ya kigaidi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Mkuu wa huduma za ambulansi mjini Mogadishu, Abdukadir Abdirahman amenukuliwa na vyombo vya habari akisema bomu lilokuwa limetegwa ndani ya gari lililenga msafara wa magari yenye uwezo wa kuzuia risasi katika mtaa wa Avisone. 

Wakazi wa Mogadishu wanasema bomu hilo lilikuwa na nguvu kiasi kwamba watu walikuwa wakisali ndani ya msikiti uliokaribu walihisi mtikisiko huku nyumba kongwe katika eneo hilo zikiwa zimeporomoka.

Kundi la kigaidi la Al Shabab linalofungamana na mtando wa Al Qaeda limetangaza kuhusika na shambulizi hilo. Kundi hilo limesema msafara ambao umelengwa ulikuwa wa 'maafisa wa kigeni'.

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 baada ya kuangushwa utawala wa Siad Barre. Katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa Al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wanaokadiriwa kufikia 21,000 wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007 ili kujaribu kukabiliana na magaidi wa al-Shabab. Hatahivyo pamoja na vitihada hizo za kimataifa, magaidi wa al-Shabab wanaendelea kutekeelza hujuma Somalia na nchi jirani ya Kenya.

3477349

captcha