IQNA

13:04 - January 16, 2022
Habari ID: 3474814
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hissen Brahim Taha amelaani vikali hujuma ya kigaidi Somalia ambayo ilipelekea karibu watu 8 wapoteze maisha.

Akitoa salamu zake za rambi rambi kwa familia, Brahim Taha amewatakia waliojeruhiwa ahueni ya haraka.

Amesema OIC inalaani kila aina ya ugaidi na inaunga mkono jitihada za Somalia katika kukabiliana na hujuma kama hizo.

Watu wasiopungua 10 waliuawa Januari 12 katika hujuma ya kigaidi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Wakazi wa Mogadishu wanasema bomu hilo lilikuwa na nguvu kiasi kwamba watu walikuwa wakisali ndani ya msikiti uliokaribu walihisi mtikisiko huku nyumba kongwe katika eneo hilo zikiwa zimeporomoka.

Kundi la kigaidi la Al Shabab linalofungamana na mtando wa Al Qaeda limetangaza kuhusika na shambulizi hilo. Kundi hilo limesema msafara ambao umelengwa ulikuwa wa 'maafisa wa kigeni'.

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 baada ya kuangushwa utawala wa Siad Barre. Katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa Al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wanaokadiriwa kufikia 21,000 wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007 ili kujaribu kukabiliana na magaidi wa al-Shabab. Hatahivyo pamoja na vitihada hizo za kimataifa, magaidi wa al-Shabab wanaendelea kutekeelza hujuma Somalia na nchi jirani ya Kenya.

4028924

Kishikizo: somalia ، amisom
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: