IQNA

Shiriki Mashindano ya Qur'ani ya Meshkat, mshindi kupata dola elfu

19:32 - January 12, 2022
Habari ID: 3474797
TEHRAN (IQNA)- Mashidano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat yatafanyika kwa njia ya intaneti ambapo washiriki watatakiwa kumuiga msomaji maarufu wa Qur'ani Marhum Sheikh Abdul Basit Abdul Swamad.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanalenga kuwahimiza vijana Waislamu duniani wajihusishe katika usomaji wa Qur'ani. Aidha mashindano hayo yanalenga kutafuta vipaya vipya katika qiraa ya Qur'ani Tukufu na hivyo yako wazi kwa watu wote.

Washiriki wanapaswa kujirekodi sauti zao na kufuata maelezo yaliyo katika tovuti ya Kiarabu ya https://mqmeshkat.com/ar/view_post/33 au ya Kiingereza ya https://mqmeshkat.com/en/view_post/33. Halikadhalika unaweza kuwasiliana na wahusika kupitia barua pepe ya MQMeshkat.ir@gmail.com. 

Wakati wa kujirekodi na kutuma klipu ni kuanzia Januari 3 hadi Februari 3 2022.  Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya dola  elfu moja huku atakayeshika nafasi ya pili akitunukiwa zawadi ya dola mia saba na wa tatu atapata zawadi ya dola mia tano.

Washiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuiga sauti ya Sheikh Abdul Basit ya Sura Al Qiyamah kama ilivyo katika klipu hii hapa chini anaposoma aya za 1-4 za Sura Al Qiyamah.

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha