IQNA

Muhula wa kushiriki Mashindano ya Qur'ani ya Meshkat waongezwa

17:46 - February 06, 2022
Habari ID: 3474899
TEHRAN (IQNA) Muhula wa kushiriki Mashidano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Meshkat yatafanyika kwa njia ya intaneti umeongezwa kwa siku tisa.

Muhula wa kujirekodi na kutuma klipu kwa wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo ulikuwa kkuanzia Januari 3 hadi Februari 3 2022. Sasa siku ya mwisho ya kutuma klipu itakuwa Februari 11.

Muhula huo umeongezwa kufuatia ongezeko kubwa la waliotaka kupewa fursa ya kushiriki mashindano hayo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanalengwa kuwahimiza vijana Waislamu duniani wajihusishe katika usomaji wa Qur'ani. Aidha mashindano hayo yanalenga kutafuta vipaya vipya katika qiraa ya Qur'ani Tukufu na hivyo yako wazi kwa watu wote.

Washiriki wanapaswa kujirekodi sauti zao na kufuata maelezo yaliyo katika tovuti ya Kiarabu ya https://mqmeshkat.com/ar/view_post/33 au ya Kiingereza ya https://mqmeshkat.com/en/view_post/33. Halikadhalika unaweza kuwasiliana na wahusika kupitia barua pepe ya MQMeshkat.ir@gmail.com.

 Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya dola  elfu moja huku atakayeshika nafasi ya pili akitunukiwa zawadi ya dola mia saba na wa tatu atapata zawadi ya dola mia tano.

Washiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuiga sauti ya Sheikh Abdul Basit ya Sura Al Qiyamah kama ilivyo

4032408

captcha