IQNA

Watu wa Morocco wanataka Misahafu irejeshwe misikitini

10:54 - January 14, 2022
Habari ID: 3474805
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Morocco wametoa wito kwa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini humo irejeshe Misahafu katika misikiti ya nchi hiyo.

Misahafu iliyondolewa katika misikiti yote ya Morocco kama njia ya kuzuia maambukizi ya COVID-19. Sasa wanaharakati wa Morocco wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii wakitaka Misahafu irejeshwe misikitini.

Abdul Samad Mukhlis, ambaye ni miongoni mwa wanaharakati, anasema misikiti ilifunguliwa miezi kadhaa iliyopita baada ya kupungua maambukizi ya COVID-19 lakini wakuu wa nchi wamezuia Misahafu kurejeshwa jambo ambalo limewanyima waumini fursa ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Hivi sasa waumini wanalazimika kusoma aya za Qur'ani kupitia simu zao za mkononi jambo ambalo linawasabishia wengi matatizo ya macho.

4028347

Kishikizo: morocoo ، misahafu ، qurani tukufu ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha