Katika muendelezo wa uungaji mkono wa kimataifa kwa Wapalestina, jana Ijumaa wananchi wa miji 56 ya Morocco walifanya maandamano 105 katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, na kusisitiza uungaji mkono wao madhubuti kwa mhimili wa Muqawama na kadhia ya Palestina.
Waandamanaji hao pia wamelaani mpango walioutaja kuwa wa fedheha wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuwafurusha Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza ili kuzima azma yao ya kutaka kuundwa kwa taifa huru la Palestina.
Maandamano haya yanafanyika katika hali ambayo, serikali ya Morocco bado haijachukua msimamo thabiti dhidi ya mauaji ya kimbari ya Wapalestina huko Gaza.
Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kukubali kurejesha uhusiano na Israel mwaka 2020 baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan.
Wananchi wa Morocco wamejiunga na wenzao katika nchi za Kiarabu kupinga vikali uamuzi wa serikali zao kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel na wametaka mapatano ya kuanzisha uhusiano huo yafutwe.
Mpango huo wa kikoloni wa Trump kuhusu Gaza unaendelea kulaaniwa duniani kote.
3491866