IQNA

Waislamu Ufaransa wanabaguliwa katika elimu ya juu

22:28 - February 18, 2022
Habari ID: 3474943
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wenye majina ya Kiislamu Ufaransa wanabaguliwa wakati wanapowasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu nchini humo.

Hayo ni kwa mujibu wa utafiti ambao umefanywa hivi karibuni na Halmashauri ya Kuchunguza Ubaguzi na Usawa Katika Elimu ya Juu Ufaransa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Gustave-Eiffel. Katika uchunguzi barua pepe 1,800 zilitumiwa Machi 2021 kwa wakurugenzi wa elimu 607 katika vyuo vikuu 19 ili kubaini iwapo wanawabagua watu walemwavu au wenye asili ya kigeni.

Uchunguzi huo umefanywa na watafiti ambao walijipachika majina bandia ambapo imebainika kuwa watu wasio na asili ya Ulaya wanabaguliwa.

Uchunguzi huo umebaini kuwa asilimia 12.3 ya wale wenye majini ya Kiislamu hupuuzwa wanapoomba kujiunga na vyuo vikuu. Kiwango hicho ni asilimi 33.3 kwa wanaotaka kusoma sheria, asilimi 21.1 kwa wanaowasilisha mamombi katika taaluma za sayansi, teknolojia na afya na asilimi 7.3 kwa wale wanaotaka kusoma lugha, fasihi na sayansi za jamii.

Tangu Rais Emmanuel Macron aliposhika hatamu za uongozi nchini Ufaransa, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na hata kuvunjiwa heshima matukufu ya  Uislamu vimeongezeka mno katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

Hivi karibuni  kamati maalumu ya Bunge la Kitaifa la Ufaransa iliidhinisha sheria ya 'thamani za jamhuri' ambazo zilipendekezwa na rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

3477855

captcha