IQNA

Al Azhar yakosoa kutiliwa shaka tukio la Mi’raj

14:16 - February 20, 2022
Habari ID: 3474950
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimetoa taarifa na kukosoa taarifa ya Mmisri mmoja aliyetilia shaka tukio la Mi’raj.

Katika taarifa, Kitengo cha Fatwa cha Kituo cha Kiislamu cha  Al Azhar  kimesema kuwa Mi’raj ni moja ya miujiza ya Mtume Muhammad SAW  na hilo limebainika wazi katika Sura za Al Isra na Al Najzm za Qur’ani Tukufu pamoja na Hadithi.

Al Azhar imesema Waislamu wote wanaafikiana kuhusu riwaya za tukio la Mi’raj na hakuna shaka katika hilo.

“Kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW ni kutaja miujiuza yake kuwa ni ndogo ni sawa na kutilia shaka nafasi ya Mtume huyo Mtukufu katika Uislamu na ni uhaini,” imesema Al Azhar.

Hivi karibuni, Ibrahim Issa akizingumza katika televisehni ya Misri alitilia shaka tukio la Mi’raj huku akidai viongozi wa kidini hawahitajiki tena katika jamii.

Al Azhar imelaani vikali matamshi hayo na kusema yanavunjia heshima dini.

Tuko la Al Isra wa Al Miraj ni safari ya usiku ya Mtume Muhammad SAW kutoka Makka hadi katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na baada ya hapo ahakaa mbinguni. Kwa ujumla, Madhehebu ya Shia na Sunni yanaafikiana kuhusu tukio la Miraj kwa kutegemea aya za Qur’ani Tukufu na Hadithi.

3477878/

Kishikizo: al azhar misri isra miraj
captcha