IQNA

Tuzo ya Mustafa SAW 2023 kupokea kazi za washiriki

21:53 - March 14, 2022
Habari ID: 3475041
TEHRAN (IQNA) – Uteuzi kwa awamu ya tano ya Tuzo ya Mustafa SAW umefunguliwa.

Sherehe za Tuzo za Mustafa SAW  2023 zitafanyika Oktoba 2023 zitafanyika amapo wasomi washindi wa tuzo hiyo  kutoka Ulimwengu wa Kiislamu watatangazwa.

Tuzo ya Mustafa(pbuh) hutolewa katika kategoria nne za Sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Sayansi ya Maisha na Tiba na Teknolojia, Sayansi ya Nano na Teknolojia ya Nano, na Sayansi ya Msingi na Uhandisi.

Katika duru hii ya Tuzo ya Mustafa SAW pia hutolewa kwa wanasayansi wanaoishi katika nchi za Kiislamu bila kujali dini zao kwa lengo la kuendeleza sayansi na teknolojia katika nchi hizi.

Tuzo hii ya aina yake katika ulimwengu wa Kiislamu  hutolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila baada ya miaka miwili kwa wasomi na wanasayansi bora wa Ulimwengu wa Kiislamu waliovumbua mambo mbalimbali katika masuala ya elimu na sayansi kwa ajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu.

Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW (The Mustafa (PBUH) Prize) ilizinduliwa mwaka 2013 na kisha ilitolewa mara ya kwanza mwaka 2015 mjini Tehran ambapo wakati huo washindi walikuwa ni Profesa Omar Yaghi wa Jordan, mtaalamu wa nanoteknolojia na Profesa Jackie Ying wa Singapore katika uga wa bio-nanoteknolojia.

Tuzo hiyo hutolewa sambamba na maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad SAW.

Waliopendekezwa wanaweza tu kuteuliwa na wanasayansi mashuhuri na/au mojawapo ya taasisi za kisayansi zifuatazo: vyuo vikuu na vituo vya utafiti, vyama vya sayansi na teknolojia na vituo vya ubora, vyuo vya sayansi na mbuga za sayansi na teknolojia.

Tuzo hizo ni pamoja na Medali ya Mustafa SAW, Cheti cha Tuzo, na zawadi maalum ya fedha taslimu ambayo hutolewa kutoka kwa wakfu wa sayansi na teknolojia, na hadi sasa zaidi ya wafadhili 400 kutoka nchi tofauti kama wanachama wa Khadem Al-Mustafa SAW wamekuwa wakiunga mkono  harakati hii ya kisayansi na kitamaduni.

Tarehe ya mwisho ya uteuzi ni tarehe 31 Agosti 2022.

Kwa habari zaidi kuhusu vigezo na kuwasilisha uteuzi, tembelea www.mustafaprize.org

3478135/2023

captcha