IQNA

Sweden yaendelea kuhushudia maandamano baada ya Qur'ani Tukufu kuvunjiwa heshima

12:16 - April 18, 2022
Habari ID: 3475138
TEHRAN (IQNA)- Waislamu na wapenda haki nchini Sweden wameendeleza maandamano kwa siku ya nne mfululizo kulalamikia mpango wa kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu nchini humo.

Rasmus Paludan, raia wa Denmark ambaye ni kinara wa chama chenye misimamo mikali cha Stram Kurs nchini Sweden aliteketeza moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wenye Waislamu wengui siku ya Alhamisi.

Paludan, akiwa ameandamana na maafisa kadhaa wa polisi, alienda katika uwanja uliowazi katika mji wa Linkoping kusini mwa Sweden ambapo alitekeleza kitendo hicho kiovu. Pludan pia alikuwa amepanga kuteketeza nakala za Qur'ani katika miji kadhaa ya Sweden wakati wa siku kuu ya pasaka.

Kufuatia jinai hiyo, kumeibuka maandamano katika miji mbali mbali ya Sweden ikiwemo Stockholm, Linköping, Landskrona, Malmo na Norrkoping ambapo waandamanaji wamepinga vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na njama ya kukariri kitendo hicho. Watu kadhaa wamejeruhiwa na magari yameteketezwa moto katika maandamano hayo. 

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha makumi ya waandamanaji waliojifunika nyuso zao wakitoa nara za "Allahu Akbar" dhidi ya kiongozi wa chama hicho kinachopiga vita Uislamu nchini Sweden.

Makundi yanayounga mkono kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu pia yamejitokeza katika maandamano ambapo inadokezwa kuwa wafuasi wa makundi hayo yenye misimao mikali ndio wanaoteketeza moto magari katika maandamano.

Mkuu wa Polisi ya Sweden, Anders Thornberg amesema hajawahi kuona maandamano kama hayo nchini humo.

Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq zimelaani vikali vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden.

4050054

captcha