IQNA

Hotuba ya Sala ya Idul Fitr Tehran
15:22 - May 03, 2022
Habari ID: 3475200
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Idul Fitr mjini Tehran amesema katika hotuba zake kwenye Swala ya Eidul-Fitri leo hapa mjini Tehran kwamba, maandamano ya Sikuu ya Kimataifa ya Quds yameonyesha kuwa, malengo matukufu ya taifa madhulumu la Palestina yangali hai.

Ayatullah Kadhim Siddiqi amesema kuwa, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds wananchi wa Iran na wa mataifa mengine ya Kiislamu walijitokeza  na kuuonyeshah ulimwengu kwamba, baada ya miaka miwili ya mazingira ya dunia yaliyotawaliwa na virusi vya Corona hakuna jambo lolote linaloweza kufifiliza kadhia ya Palestina.

Ayatullah Siddiqi ameongeza kuwa, malengo ya ukombozi wa Quds (Jerusalem) na Palestina kwa ujumla yako hai na operesheni za kujitolea shahidi za vijana shupavu wa Kipalestina zimebinya medani ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikoloni ardhi hizo za Wapalestina.

Aidha amesema, kusimama kidete Wapalestina hii leo kumeufanya utawala wa Kizayuni wa Israel kuondoka katika hali ya hujuma na mashambulio na kukumbwa na hofu na wahaka mkubwa na muda si mrefu utasambaratika.

Khatibu wa Sala ya leo ya Eidul Fitri hapa mjini Tehran ameashiria matukio ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Afghanistan na undumakuwili wa madola yanayodai kutetea haki za binadamu kuhusiana na matukio ya Afghanistan, Ukraine na Yemen na kusema kuwa, wanaodai kutetea haki za binadamu ni warongo wakubwa.

Kadhalika ameitolea witoserikali inayotawala nchini Afghanistan kudumisha usalama kwa ajili ya wananchi sambamba na kuwasaka na kuwashughulikia wanaohusika na vitendo vya mauaji dhidi ya raia wasio na hatia yoyote.

4054576

Kishikizo: idul fitr ، tehran ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: