IQNA

Hujuma ya Israel dhidi ya mazishi ya mwanahabari shahidi Abu Akleh

17:18 - May 14, 2022
Habari ID: 3475248
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limetenda jinai nyingine kwa kuushambulia kinyama mkusanyiko wa kuusindikiza mwili wa shahidi Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa kanali ya Televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.

Mkusanyiko huo waombolezaji ulishambuliwa na wanajeshi wa Israel Ijumaa huku ukiwa umebeba jeneza la mwanahabari huyo huku waombolezaji wakivumilia vipigo vya wanajeshi hao lakini jeneza lisianguke.

Video ya tukio hilo la kinyama inayowanoyesha wanajesi wa Israel wakiwashambulia na kuwapiga waombolezaji waliobeba jeneza la Shireen Abu Akleh nje ya hospitali imewawazunisha mno walimwengu.

Mandhari hiyo imeonyesha ni kwa kiwango gani wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walivyokuwa makatili kwani hawakuwa na huruma hata kwa maiti ya mwanahabari huo.

Kitendo hicho cha wanajeshi wa Israel kilipelekea kutokea mapigano baina yao na Wapalestina waliokuwa wakijitahidi kuwazuia wanajeshi hao wasiwashambulie wabeba jeneza ambapo wakati mwingine jeneza hilo lilikaribia kuanguka chini kutokana na mashambulio hayo ya Israel.

Jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu, mataifa na asasi mbalimbali za kieneo na kimataifa zimetoa taarifa ya kulaani unyama na ukatili huo wa wanajeshi wa Israel.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa ya kulaani jinai na hujuma hiyo ya Israel dhidi ya mkusanyiko wa Wapalestina waliokuwa waklienda kumzika Shireen Abu Akleh, ripota mahiri na mashuhuri wa televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.

Mapema Jumatano, mwandishi wa habari ya televisheni ya al Jazeera, Shireen Abu Akleh, 51, alipigwa risasi na kuuliwa shahidi kikatili na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati akiwa kwenye kazi yake ya kuripoti uvamizi wa kijeshi wa jeshi la Israel katika kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin.

Jinai hiyo inaendelea kulaaniwa kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakitaka utawala huo wa Kizayuni ufikishwe kizimbani.

 Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri baada ya kufanyika uchunguzi kuwa, Shireen Abu Akleh aliuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo.

4056624

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :