IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina wataka Israel iadhibiwe kwa kumuua Abu Akleh

21:37 - September 06, 2022
Habari ID: 3475745
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS amezungumzia ripoti ya jeshi la utawala wa Kizayuni baada ya utawala huo katili kumuua shahidi mwandishi Mpalestina, Shireen Abu Akleh na sawa na Wapalestina wote, ametaka utawala huo dhalimu upewe adhabu kali.

Hazem Qassem akisema hayo na kuongeza kuwa, uchunguzi uliofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni ni njama mpya za kujaribu Israel kukwepa kubeba jukumu la jinai yake ya kumuua kigaidi mwandishi wa habari Shireen Abu Akleh wakati ushahidi wote unaonesha kuwa mauaji hayo ni katika jinai za kivita zinazotendwa kila leo na wanajeshi wa makatili wa utawala wa Kizayuni.

Mwezi Julai mwaka huu pia, Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina ililalamikia pia ripoti ya Marekani kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa al Jazeera, Shireen Abu Akleh na kusema kuwa ripoti ya dola hilo la kibeberu ilichapishwa kwa shabaha ya kuuondoa hatiani na kuficha jinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwezi huo wa Julai, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilidai katika ripoti iliyolenga kuiondolea mashtaka Tel Aviv kwamba "Shireen Abu Akleh huenda aliuawa bila kukusudia kwa risasi iliyotoka upande wa wanajeshi wa Israel."

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ilisisitiza katika taarifa yake kwamba, ripoti ya upendeleo ya Marekani kuhusu utawala wa Kizayuni wa Israel imetolewa ndani ya fremu ya mienendo ya kawaida ya Marekani ya kumuunga mkono adui Mzayuni, na hata inaweza kusemwa kuwa, Washington inahusika katika mauaji na ugaidi unaofanywa dhidi ya wananchi wa Palestina kupitia misaada yake ya silaha za aina mbalimbali kwa utawala huo ghasibu.

Shireen Abu Akleh aliyekuwa na umri wa miaka 51, ripota wa televisheni ya al Jazeera yenye makao yake nchini Qatar, aliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel tarehe 11 mwezi Mei mwaka huu wakati akiripoti  uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina. 

4083569

captcha