IQNA

19:19 - May 14, 2022
Habari ID: 3475251
TEHRAN (IQNA)- Aliyekuwa nyota wa timu ya Soka ya Cameroon, Patrick Mboma amesilimu leo na kuchagua jina la Abdul-Jalil ambalo atalitumia akiwa Mwislamu.

Hafla ya kusilimu na kutamka shahada mbili mwanasoka huyo ilifanyika Ijumaa hii katika msikiti wa Bonamoussadi huko Douala katika tukio ambalo limehudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu.

Mboma ambaye alikuwa katika timu ya taifa ya soka ya Cameroon maarufu kama Indomitable Lions katika uchukua ubingwa wa Afrika mara  mbili (2000-2002) aliicheza timu hiyo mara 56 na kufunga mabao 33.

Hatua ya Mboma kuchagua Uislamu kama njia ya maisha imekuja  miezi michache baada ya  nyota mwingine wa soka Clarence Seedorf wa Uholanzi naye kusilimu.

Mboma mwenye umri wa miaka 51 amewahi pia kuchezea vilabu maarufu Ulaya  kama vile Paris Saint Germain na ana shahad ya uzamili katika ukocha.

 

ستاره سابق تیم ملی فوتبال کامرون به اسلام گروید + فیلم

4056905

Kishikizo: amesilimu ، mboma ، uislamu ، cameroon
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: