IQNA

Waislamu India
17:36 - May 19, 2022
Habari ID: 3475267
TEHRAN (IQNA)- Mahakama Kilele ya India imebatilisha uamuzi wa mahakama ya chini ambayo ilikuwa imeamuru marufuku ya sala za jamaa katika msikiti wa Karne ya 17 kaskazini mwa India kwa madai kuwa kulikuwa na mabavu ya mmoja ya miungu ya Kihindu, Shiva, na nembo zingine za Kihindu hapo.

Katika hukumu iliyotolewa Jumanne, mahakama  hiyo imeamuru kuendelea Sala za Waislamu katika Msikiti wa Gyanvapi jimboni Uttar Pradesh na kwamba mabaki ya dini ya Kihindu yanayodaiwa kupatikana hapo yalindwe. Kesi hiyo itaendelea Jumanne.

Yanayojiri hapo ni sawa na yali yaliyojiri Disemba sita mwaka 1992, wakati Wahindu wenye misimamo mikali waliubomoa Msikiti wa Babri katika mji wa Faizabad kwa lengo la kujenga hekalu la ram, mmoja wa miungu ya Kihindu. Katika hujuma hiyo Waislamu zaidi ya 2,000 waliuawa. 

Hukumu hiiyo kuuhusu Msikiti wa Gyanvapi inakuja huku Wahindu wenye misimamo mikali nchini India wakiteteketeza moto msikiti katika kati mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Jang la Pakistan, Wahindu wenye misimamo ya kufurutu adha wameteketeza moto msikiti katika  mji wa Nemuch katika jimbo la Madhya Pradesh. Taarifa zinasema Wahindu wenye misimamo mikali pia wamevurumisha mawe katika nyumba za Waislamu katika jimbo hilo na kuwajeruhi Waislamu kadhaa. 

Katika upande mwingine, katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, mwanamke Muislamu aliyekuwa na umri wa miaka 53 alipigwa risasi na kuuawa na polisi wakati akijaribu kuzia mwanae wa kiume kukamatwa kwa kosa la kuchinja ng'ombe.

Hivi karibuni katika eneo la Karauli jimboni Rajasthan  nyumba 40 za Waislamu ziliteketezwa moto na Wahindu wenye misimamo mikali.

Katika mwezi wa Aprili 2022 pia katika sherehe ya Kihindu ya "Ram Navami" katika jimbo la Madhya Pradesh, mamia ya nyumba za Waislamu jimboni humo ziliharibiwa na mabuldoza yaliyokuwa yakiendeshwa na Wahindu wenye misimamo mikali. Picha za familia zisizo na yumba na watoto waliokuwa wakilia baada ya jinai hiyo zilisambazwa katika mitandao ya kijamii na kulaaniwa kieneo na kimataifa.

Kuteketeza moto msikiti, ambalo ni eneo takatifu kwa Waislamu, si jambo jipya nchini India.

Katika miongo ya hivi karibuni idadi kubwa ya misikiti nchini India imeharibiwa, kuteketezwa moto au kuhujumiwa na Wahindu wenyemisimamo mikali. Waislamu wengi wameuawa au kujeruhiwa katika hujuma hizo za Wahindu. Kwa kawaida jinai hizo hujiri baada ya hotuba za Wahindu wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

3478958

 

Kishikizo: Gyanvapi ، india ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: