IQNA

Uislamu na vita dhidi ya njaa
22:48 - May 23, 2022
Habari ID: 3475286
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi ametoa wito kwa maafisa wa nchi hiyo kuchukua somo kutoka aliyoyasema Nabii Yusuf AS katika Qur’ani Tukufu kuhusu kuweka akiba ili waweze kushughulikia hali ya sasa ya uhaba wa ngano na nafaka zingine.

Katika miezi ya hivi karibuni, wasiwasi umeenea ulimwenguni kote kutokana na ukosefu wa chakula, na bei ya ngano na nafaka zingine zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 katika kipindi cha mwezi moja..

Misiri, ambayo ni kati ya watumiaji wakuu wa ngano ulimwenguni, imeathiriwa na uhaba wa bidhaa hiyo na inatafuta njia za kushughulikia hali hiyo.

Akihutubia sherehe ya kuzindua mradi mkubwa wa kilimo Jumamosi, El-Sisi alitaja suala hilo na akasema Misri inakabiliwa na changamoto baada ya kuongezeka kwa bei ya nafaka kutokana na oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine.

Rais wa Misri ameashiria ya 47 ya Surah Yusuf katika Qur’ani Tukufu isemayo:  “Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni katika mashuke yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula.”

 El-Sisi amewataka Wamisri wafuate  mbinu  hii ya Nabii Yusuf  ambayo ni funzo kuhusu kukabiliana na shida ya chakula na kuongeza usalama wa chakula kwa nchi.

Misiri inahitaji tani milioni 23 za ngano kila mwaka lakini inazalisha tani milioni 9 na hivyo inalazimika kuagiza kutoka nje ili kukidhi mahitaji yake.

4059038

Kishikizo: misri ، waislamu ، nabii yusuf ، nafaka ، ngano
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: