IQNA

Msomi: Utawala wa Kiislamu unategemea akili, sheria

16:27 - March 07, 2025
Habari ID: 3480321
IQNA – Msomi wa Kiislamu kutoka Iran amesema Qur’ani Tukufu ina mfundisho yenye thamani kubwa na yenye faida kwa utawala katika jamii.

Hujjatul Islam Seyed Mohammad Hassan Abutorabifard amesema kwamba kulingana visa vya kweli katika sura mbili za Qur’ani yaani Sura Yusuf na Sura Naml, kuhusu maisha ya Nabii Yusuf (AS) na Nabii Suleiman (AS), mtu anaweza kufikia natija kwamba kanuni za utawala zimejengwa juu ya miongozo ya Qur’ani, zikiwa zina misingi ya hekima na sheria.

Alitoa maoni hayo katika hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya 32 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran siku ya Jumatano.

Alisema Qur’ani Tukufu imetoa mwongozo kuhusu  usimamizi wa masuala ya kisiasa ya jamii, na inatarajiwa kwamba wasomaji wake, wahifadhi, na wafuasi waaminifu watafuta mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuchukua fursa ya mwezi wa Ramadhani kujipamba na mafundisho ya Qur’ani.

Hujjatul Islam Abutorabifard alirejelea moja ya maeneo muhimu yaliyotajwa katika Qur’ani Tukufu ambayo yana jukumu kuu katika mabadiliko ya jamii za binadamu, akisema eneo husika ni utawala.

Qur’ani Tukufu ina hazina kubwa ya maarifa ambayo wasimamizi wakuu, wa kati, na wa chini katika jamii wanapaswa kuzingatia kwa makini, kulingana na mafundisho haya, alisisitiza.

“Hili ni muhimu kwa kuzingatia maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuhusu ulazima wa kusonga mbele zaidi ya hatua zilizopigwa katika Mapinduzi ya Kiislamu na kujenga mfumo bora wa Kiislamu.”

Akiashiria Sura Yusuf ,alitathmini mafundisho yaliyowasilishwa katika sura hii kama vidokezo muhimu na alama kuu katika uwanja wa utawala.

Alisema kwamba watawala na watoa maamuzi wanaweza kutegemea maarifa yaliyotolewa katika Sura hii ili kufungua njia ya kuanzisha mfumo wa kisiasa.

Sura hii inaelezea nabii anayepitia mateso makubwa na majaribu katika maisha yake yote, alibainisha.

“(Yusuf) anatupwa kwenye kisima, anatupiwa lawama nyingi, na mwishowe anawekwa gerezani. Hata hivyo, mtu lazima afikirie ni hali gani na falsafa gani ilimuwezesha kufika nafasi ya juu zaidi ya serikali ya Misri baada ya kipindi kirefu cha mabadiliko, na ni vigezo gani vinavyosimamia uteuzi huu.”

Hujjatul Islam Abutorabifard amesisitiza kwamba kuwepo kwa mfalme anayesimamia serikali ya Misri, ambaye alitafuta ukweli na haki, kulikuwa na jukumu muhimu, licha ya ukweli kwamba jamii ya Misri ilikuwa ikipitia ushirikina na ilikuwa mbali na imani za imani ya Mungu mmoja.

“Pamoja na hayo, alifuata sheria, ambayo ilirahisisha tukio hili, kumruhusu mtu ambaye alikuwa ameshtakiwa isivyo haki kufikia nafasi ya maamuzi katika utawala wa Misri,” aliendelea kusema.

3492199

 

captcha