IQNA

Jinai za Marekani

Marekani Marekani haina ustahiki wa kuzungumza kuhusu hali haki za binadamu

12:23 - July 04, 2022
Habari ID: 3475461
TEHRAN (IQNA)- Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani haina ustahiki wa kuzungumzia suala la haki za binadamu kutokana na namna inavyokiuka kwa wingi haki za binadmau duniani.

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran Kazem Gharibabadi amesisitiza kuwa Marekani, kwa vyovyote vile, haina sifa ya kuzungumzia suala lahaki za binadamu.

Afisa huyo ametoa tamko hilo akizungumzo katika Kongamano la Nne la Kimataifa wa Haki za Binadamu za Kimarekani kwa Mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.

Gharibabadi aliongeza aliongeza kuwa, "Marekani inapaswa kuwajibishwa kuhusu watu wanaokandamizwa, ambao wamepoteza maisha kutokana na ugaidi, vikwazo, uchokozi na uvamizi,"

Alitoa mfano wa watu wa Yemen ambao wanakabiliwa vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia na washirika wake, vita ambavyo vinaungwa mkono na Marekani. Wayemeni bado wananyimwa msaada wa kimsingi zaidi wa kibinadamu kutokana na wavamizi na waaungaji mkono wao ambao wana "tabia ya ubeberu na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu," afisa huyo alibainisha.

Akihutubia mkutano huo, Naibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika Masuala ya Kisiasa, Ali Baqeri-Kani alisema kukanyaga haki za binadamu za watu huru ni "sehemu na sehemu" ya sera ya nje ya Marekani.

Amesema, "Mtu anaweza kusema kwa ujasiri kwamba hakuna taifa katika dunia ya leo ambalo halijaonja ladha chungu" ya hakki za binadamu kwa mtazamo wa Marekani."

‘Baqeri-Kani amesema "vikwazo na ugaidi" ni nguzo kuu za haki za binadamu za Kimarekani na kuongeza, "Ikiwa watanyang'anywa nguzo hizi mbili, wanaweza wasiweze kuendelea na satwa yao ya kibeberu na njama dhidi ya wengine.

Katika kalenda ya Iran tarehe 27 Juni hadi tatu Julai hutambuliwa kama Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani ambapo katika wiki hii utambulisho halisi wa jinai za Marekani hubainishwa wazi mbele ya walimwengu na hivyo kufichua hadaa ya Marekani katika madai yake kuwa eti ni mtetezi wa haki za binadamu. Katika wiki hii pia huangaziwa zaidi jinai za Marekani dhidi ya Wairani wasio na hatia.

Kati ya jinai hizo za Marekani dhidi ya watu wa Iran ni tukio la Tarehe 28 Juni, 1987 utawala wa Saddam wa chama cha Baath nchini Iraq ulitumia mabomu ya kemikali kushambulia maeneo manne ya mji wa Sardasht  nchini Iran yaliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu. Katika shambulio hilo la kinyama, raia  110 wa mji huo waliuawa shahidi na wengine 8,000 waliathirika kwa gesi ya sumu ya silaha hizo. Nchi za Magharibi, hasa Ujerumani, Uingereza na Marekani ndizo zilizompa Saddam silaha hizo za kemikali. 

Jinai nyingine ya Marekani dhidi ya watu wa Iran ni  ile ya miaka 34 iliyopita ya Julai 3, 1988, ambapo meli ya kivita ya Marekani ya Vincennes ilivurumisha kombora dhidi ya ndege ya abiria ya Iran Aira aina ya Airbus iliyokuwa ikiruka kutoka Bandar Abbas kuelekea Dubai. Katikak jinai hiyo, abiria wote 290, wakiwemo watoto 66 na wanawake 53, waliuawa kinyama kutokana na uamuzi uliochukuliwa na nahodha wa manowari ya Vincennes wa kutungua kwa kombora ndege hiyo ya abiria ya Iran. Kati ya abiria hao, 254 walikuwa Wairani, 13 raia wa Umoja wa Falme za Kiarabu, kumi walikuwa Wahindi, sita Wapakistani, sita raia wa Yugoslavia na mmoja Mwitaliano.

Katika kukumbuka jinai hizo za Marekakni, kkatika kalenda ya Iran tarehe 27 Juni hadi tatu Julai hutambuliwa kama Wiki ya Haki za Binadamu za Kimarekani ambapo katika wiki hii utambulisho halisi wa jinai za Marekani hubainishwa wazi mbele ya walimwengu na hivyo kufichua hadaa ya Marekani katika madai yake kuwa eti ni mtetezi wa haki za binadamu. Katika wiki hii pia huangaziwa zaidi jinai za Marekani dhidi ya Wairani wasio na hatia.

4068316

Kishikizo: gharibabadi ، sardasht ، marekani ، jinai ، iran ، Vincennes
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :