IQNA

Jinai za Marekani

Kauli ya Imam Khomeini baada ya Marekani kutungua ndege ya abiria ya Iran

12:12 - July 04, 2022
Habari ID: 3475460
TEHRAN (IQNA) Tarehe 3 kila mwaka nchini Iran Julai ni siku ya kumbukumbu ya shambulio la kombora lililofanywa na meli ya kivita ya Marekani ya Vincennes dhidi ya ndege ya abiria ya Iran aina ya Airbus iliyokuwa ikiruka kutoka Bandar Abbas kuelekea Dubai.

Baada ya  jinai ya Marekani ya kutungua ndege ya abiria ya Iran na kuuawa shahidi watu 290 wasio na hatia, Imam Khomeini (radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie) alitangaza katika ujumbe wake huku akitoa pole kwa msiba huu: “Vita vyetu ni vita vya itikadi yetu dhidi dhuluma; vita vyetu ni vita vya Kiislamu. Ni dhidi ya kukosekana kwa usawa kwa ulimwengu wa ubepari na Ukomunisti ... Vita hivi ni vita vya Imani, vita vya maadili ya kidini-mapinduzi dhidi ya dunia inayotumia mabavu, fedha na anasa."

Baada ya kutunguliwa ndege hiyo, watawala wa Marekani walitoa sababu zilizogongana wazi za kujaribu kuhalalisha jinai hiyo usiyosameheka na kuonyesha kuwa kitendo hicho cha uadui kilifanyika kimakosa, lakini kwa kuzingatia kwamba meli ya vita ya Vincennes ilikuwa na vifaa na mifumo ya kisasa kabisa ya rada na pia kutambulika wazi ndege iliyokuwa angani, ilibainika wazi kuwa hakukuwepo na uwezekano wa kufanyika kosa katika mazingira hayo na kwamba hiyo ilikuwa hatua iliyochukuliwa kwa makusudi na adui kwa madhumuni ya kusababisha maafa na hasara dhidi ya taifa la Iran.

Jana wananchi wa Iran zikiwemo familia za wahanga wa ukatili huo wamekusanyika katika eneo la baharini mkoani Hormuzgan kwa ajili ya kumbukumbu ya umwagaji damu huo, huku wakipiga nara za 'Mauti kwa Marekani' na 'Mauti kwa Israel.'

Shambulio hilo lilidhihirisha zaidi unyama na ukatili unaotekelezwa na serikali ya Marekani. Viongozi wa Marekani walizidisha ukatili wao huo pale walipomzawadia medali ya eti ya ushujaa nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho cha kigaidi.

Kutunguliwa ndege ya abiria ya Iran na manowari ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kuuawa shahidi abiria wake ni moja ya maafa yasiyosahaulika katika historia ya mwanadamu na aibu ya milele kwa wale wanaodai kutetea haki za binadamu duniani.  Bila shaka jinai hiyo iliyosababisha majeraha makubwa yasiyopona kwenye nyoyo za wapigania uhuru na ukweli ulimwenguni, ilithibitisha kwamba Marekani ambayo inadai kutetea haki za binadamu na kupambana na ugaidi duniani, yenyewe ni miongoni mwa wavunjaji wakubwa wa haki za binadamu na mmoja wa waungaji mkono wakuu wa ugaidi kimataifa. Halikadhalika jinai hiyo ya kutungua ndege ya abiria ni dalili ya wazi ya ugaidi wa kiserikali ambao ni sera ya dhati ya Marekani.

4068193

Kishikizo: Vincennes ، marekani ، iran ، ugaidi ، ghuba ya uajemi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :