IQNA

Maambukizi ya Covid-19

Kuvaa barakoa ni sharti kwa wanaoingizi misikitini Qatar

15:08 - July 07, 2022
Habari ID: 3475470
TEHRAN (IQNA) - Uvaaji wa barakoa ndani ya misikiti itakuwa ya lazima nchini Qatar kuanzia Alhamisi.

Hayo yametangazwa na Wizara ya Wakfu ya na Masuala ya Kiislamu katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, wizara hiyo imesema hii inatokana na uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa Jumatano unaofanya uvaaji wa barakoa kuwa wa lazima katika maeneo ya umma yaliyo katika maeneo yenye paa, ikiwa ni katika hatua za tahadhari zinazochukuliwa na nchi kupunguza kuenea kwa Covid-19

"Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailinde nchi yetu pendwa dhidi ya maovu yote na aondoe janga hili na kuondoa wingu hili kutoka kwake na kwa wanadamu wote," taarifa hiyo iliongeza.

Siku ya Jumatatu Qatar ilisajili kesi mpya 599 za Covid-19 na kwa ujumla sasa kuna watu 5,045 walioambukizwa. Kwa wastani watu 637 wamekuwa wakiambukizwa Covid-19 kila siku nchini humo. Wizara ya Afya ya Qatar imetoa wito kwa watu milioni 1.7 kote nchini humo kupata dozi ya nne ya chanjo ya Covid-19.

3479611

captcha