IQNA

Kususia utawala wa Kizayuni wa Israel

Wapalestina wampongeza mwanamichezo shujaa wa Algeria aliyekataa kucheza na Waisraeli

20:13 - July 29, 2022
Habari ID: 3475552
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wamempongeza mmoja wa wanamichezo shujaa wa Algeria ambaye amekataa kwenda kucheza mpira katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel ikiwa ni kuendeleza harakati ya kimataifa ya kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestinaa na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ahmed Touba mchezaji wa mpira wa miguu wa Algerria amekataa kufuatana na timu yake ya İstanbul Başakşehir kwenda kucheza na timu ya Wazayuni ya Maccabi Netanya FC huko Israel katika mashindano ya Ulaya.

Wananchi wa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu wanalihesabu suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni usaliti na ni sawa na kulipiga jambia kwa nyuma, taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Taarifa zinasema kuwa, hatua ya mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria, Ahmed Touba ya kukataa kwenda kucheza na Wazayuni imechukuliwa ili kuonesha uungaji mkono wake kwa taifa la Palestina na kupinga hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. Hatua hiyo imepokewa kwa shangwe na waungaji mkono wa ukombozi wa Palestina.

Ikumbukwe kuwa Algeria ni katika nchi za Kiarabu zilizoko mstari wa mbele katika kuliunga mkono taifa la Palestina na kupinga uhusiano wa kawaida na Wazayuni. 

Algiers ilisaidia sana kutimuliwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya Umoja wa Afrika baada ya hatua za awali za kujaribu kuifanya Israel kuwa mwanachama mwangalizi ndani ya AU.

3479880

Kishikizo: algeria ، mwanamichezo ، palestina ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha