Real Valladolid ilifanya mkutano na waandishi wa habari kumtambulisha Jaouab, baada ya kuhamia kutoka klabu ya Rennes ya Ufaransa. Tukio hilo lilijawa na furaha na shamrashamra za sherehe.
Mkutano huo ulianza kwa njia isiyo ya kawaida, ambapo mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Victor Orta, alisoma aya za 39 hadi 41 kutoka kwenye Surah An-Najm ya Qur’ani.
“Kwa hakika kuna aya katika Qur’ani zinazosema, ‘Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe. Na jitihada zake zitaonekana. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
Hivyo, malipo yako na mafanikio yako katika klabu hii, ambayo yatakuwa mafanikio ya kila mmoja,’’ alisema Orta."
Mlinzi huyo wa Morocco kwa upande wake alionesha azma yake na dhamira ya kutoa kila kitu ili kuchangia maendeleo ya timu, akiwa peke yake na kwa pamoja.
Jaouab alizungumza kwa Kiarabu, akisaidiwa na mkalimani. Alionesha imani yake kubwa kwa kocha, akisema, “Nina imani kubwa na kocha, na ninafanya kazi kwa bidii ili kutoa kila kitu kutoka kwangu uwanjani mara atakapochagua.”
Aliongeza, “Ninalenga kucheza ipasavyi, mwaka huu ni muhimu sana kwa Real Valladolid na nataka kufanya mazoezi vizuri zaidi ili nipate kucheza.”
Mchezaji huyo wa Morocco alielezea sababu ya kuchagua kujiunga na klabu hiyo: “Nilitaka kucheza Uhispania, na Victor alinielezea kuhusu klabu hii. Nilivutiwa sana na Real Valladolid, kwani ni klabu yenye malengo na historia nzuri pamoja na mwelekeo imara.”
Akibanisha kuhusu nguvu zake uwanjani, aliongeza, “Mimi hutegemea akili yangu uwanjani, pamoja na nguvu zangu za kimwili, lakini akili yangu ndio silaha yangu muhimu zaidi.”
Msimu uliopita, Wamorocco watatu walicheza kwa Real Valladolid: Adam Aznou, Selim Amallah, na Anuar Tuhami.
3494358