IQNA

Kupigwa marufuku mwanajudo Algeria ni ishara ya unafiki

23:44 - September 09, 2021
Habari ID: 3474278
TEHRAN (IQNA)- Mwanamichezo wa mchezo wa Judo wa Algeria, Fethi Nourine (Fat-hi Nurin), ambaye alifadhilisha kujitoa kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo kuliko kucheza na mwakilishi wa utawala haramu wa Israel, bado anaendelea kugonga vichwa vya habari.

Shirikisho la Kimataifa la Judo (IJF) limempiga marufuku Mualgeria huyo mwanamapinduzi pamoja na kocha wake na kusema hawataruhusiwa kushiriki katika michezo yoyote itakayoandaliwa na shirikisho hilo kwa muda wa miaka 10 ijayo.

Nayo Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imedai kuwa uamuzi huo wa Nourine ‘ulikiuka kanuni za Hati ya Olimpiki’.

Nourine ametoa kauli kufuatia uamuzi huo na kusema: “Ni adhabu kali lakini ilitarajiwa na ni thibitisho kuwa wanaunga mkono ugaidi  wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wetu huko Ghaza.”  Ameendelea kusema kuwa: “Kwa hakika wao ni washirika wa jinai za utawala ghasibu wa Israel. Sijakiuka sheria yoyote bali kujiondoa kwangu kulikuwa ni kitendo cha kubainisha kufungamana na Wapalestina.”

Amesema marufuku dhidi yake na kocha wake ni kitendo cha unafiki cha shirikisho hilo kwani Israeli inaruhusiw akushiriki katika michezo kama nchi ya kawaida wakati ambao inakiuka sheria na mikataba ya kimataifa. Aidha amesema hata Wapalestina Waisraeli wanabaguliwa lakini Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki inaona hilo ni jambo la kawaida.

Mwanamichezo wa Judo kutoka Algeria alitangaza kujiondoa kwenye michuano ya Olimpiki ya 2020 iliyofanyika mwaka huu wa 2021 baada ya kura ya duru ya pili ya utangulizi wa mashindano hayo katika uzito wa chini ya kilo 73 kumwangukia apambane na mshindani kutoka Israel.

Algeria, kinyume na jirani yake Morocco, ni nchi inayopinga kuanzisha uhusiano wa aina yoyote na utawala haramu wa Israel na kuendelea kushikilia kila mara msimamo wake thabiti wa kuliunga mkono taifa la Palestina.

3475667

captcha