IQNA

Kadhia ya Palestina

Algeria kuendelea kuunga mkono Palestina, Rais Tebboune asema

19:07 - September 25, 2022
Habari ID: 3475837
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune alisema suala la Palestina ndilo suala la msingi kwa nchi yake.

Hakuna "mvulana wa Algeria au mtu mzee ambaye haungi mkono Palestina," alisema.

"Palestina ni kadhia ya kitaifa kwa Algeria, na hatukubali ukoloni" ndani yake, Tebboune alisisitiza.

"Tutaendelea kuiunga mkono Palestina hata kama ilitawaliwa na mataifa yenye nguvu zaidi duniani. Palestina ni ya Wapalestina, si ya wengine.

"Tulipigana na ukoloni na kusukuma misafara ya mashahidi, na hatuwezi kukubali nchi kutawaliwa; tutapambana na ukoloni popote ulipo," alisisitiza.

Ni vyema kuashiria hapa kuwa makundi yote ya Wapalestina yatashiriki katika mkutano nchini Algeria, katika wiki ya kwanza ya Oktoba, kwa ajili ya maandalizi ya mkutano ujao wa kilele wa Jumuyia ya Nchi za Kiarabu, ambao serikali ya Algeria iliuita mwaka huu kuwa ni Mkutano wa kilele wa Palestina.

Inalenga kuunganisha safu za Waarabu katika kuunga mkono kadhia ya Palestina.

3480618

Kishikizo: palestina ، algeria ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha